MECHI YA WATANI LIGI KUU DESEMBA 11

BODI ya Ligi Tanzania, leo imetangaza rasmi ratiba ya Ligi
Kuu Tanzania huku ikionyesha kuwa pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga
ambalo huvuta hisia za watanzania wengi, litapigwa Desemba 11 mwaka huu.
Aidha, mechi za kwanza za vigogo zinaonyesha Simba wataanza
na Biashara ugenini kama ambavyo watani wao Yanga nao wataanzia Kagera huku
Azam wakiwafuata Coastal Union mjini Tanga.

Post a Comment