MABAKI YA MWILI WA MUGABE KUZIKWA UPYA MAKABURI YA MASHUJAA WA TAIFA

 Robert Mugabe: Is Zimbabwe's ex-president a hero or villain? - BBC News

MAHAKAMA Kuu ya Zimbabwe imeamuru kufukuliwa kwa mabaki ya Rais wa zamani wa nchi hiyo, hayati Mzee Robert Gabriel Mugabe ili kuzikwa tena katika makaburi ya mashujaa wa taifa.

Watoto watatu wa rais Mugabe Bona, Bellarmine na Tinotenda walikwenda mahakamani kupinga agizo la chifu wa jadi wa jamii ya Zvimba kwamba mabaki ya baba yao yazikwe katika eneo la Mashujaa katika mji mkuu Harare.

Mugabe alifariki Septemba 2019 na kuzikwa nyumbani kwake kijijini Kutama, kilomita 90 kutoka mji mkuu wa Zimbabwe Harare. 

No comments