USALITI WA MAPENZI WAUA WAWILI MLANDIZI

WATU wawili wamefariki kwa
kunywa sumu katika kitongoji cha Mlandizi kata ya Mlandizi Tarafa ya Mlandizi
Wilaya ya kipolisi Mlandizi Mkoani Pwani.
“Tarehe 5 September 2021 asubuhi
huko Mlandizi Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni Wapenzi walikutwa wamefariki katika
makazi yao baada ya kunywa kitu kinachodhaniwa ni sumu. Watu hao ni Godfrey
Pius Mandai (48) ambaye alikuwa ni dereva na Veronica Gerald ( 42)
Mfanyabiashara na mkazi wa Mtwara ambaye alisafiri kutoka Mtwara na kumfuata mpenzi
wake huyo Mlandizi.
“Mwanaume yule alitengeneza
juisi ambayo ndani yake ilikuwa na sumu akampa Veronica akanywa na kufariki,
mwanaume alipoona mpenzi wake amefariki na yeye akanywa na akafariki”
“Chanzo ni wivu wa kimapenzi
ambapo Mwanaume alikuwa anamtuhumu Veronica kuwa anafanya usaliti, kwenye eneo
la tukio tumekuta chupa yenye masalia ya sumu na tumekuta pia karatasi ambayo
inadhaniwa imeandikwa na mmoja wao na imeandikwa ‘HUU NI USALITI TU’amesema
Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa.

Post a Comment