SPIKA NDUGAI AHOFIA WASOMI KUMRARUA MITANDAONI

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amesema
anakerwa na kada nne ambazo zinatukuza usomi wao mbele ya Watanzania wasiopenda
kujikweza.
Amezitaja kada hizo ni wahasibu, wahandisi, mawakili na
madaktari wa kusomea ambao amesema kila mtu anataka kuanza na kutukuza kisomo
chake wakati si lazima iwe hivyo.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo, Jumatano, Septemba 1,
2021 bungeni katika kipindi cha mjadala wa hoja za wabunge kuhusu muswada wa
mabadiliko ya sheria mbalimbali uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Profesa Adelardus Kilangi.
Amesema anajua atashambuliwa na mawakili mitandaoni lakini
anataka kujua iwapo hawaoni aibu kujiita ni wasomi wakati nchi ina wasomi
wengine.
“Najua watanishambulia katika mitandao, ..ah lakini huo ndiyo
ukweli nani asiyekuwa msomi katika nchi hii, au wengine hawajasoma, kwani
hamuoni aibu fulani hivi kujiita wasomi wakati kuna wengine katika nchi hii
wamesoma,” amehoji Ndugai.
Spika amesema; “kuna wakati nitahitaji mnishauri kuhusu hili
la wanasheria kujiita wakili msomi, huu ni utaratibu fulani ulioanzishwa na
wenzetu Waingereza wa kutukuza baadhi ya kada,’’
Ndugai amezitaja kada nne zinazompa shida na anawashangaa
kuona wakitukuzwa kuliko wengine licha ya wengi kuwa ni wasomi.
Kada hizo ni wahasibu, wahandisi, mawakili na madaktari wa
kusomea ambao amesema kila mtu anataka kuanza na kutukuza kisomo chake wakati
siyo lazima iwe hivyo.
Kuhusu mawakili amehoji kama wakibaki na neno la wakili
watapungukiwa kitu gani huku akiweka wazi kuwa neno msomi linawaongezea kitu
gani kwa Watanzania wasiopenda kujikweza katika mambo mengine.
Kwa kada alizozitaja Spika, mawakkili hujiita wakili msomi,
wahasibu hupenda kuanza na neno CPA, wahandisi hutumia neno la ‘Engineer’ na
waliosoma shahada za uzamivu (PhD) majina yao huanza na neno Dk

Post a Comment