SAFARI ZA NDEGE ZAREJEA TENA AFGHANISTAN

SAFARI za ndege za kimataifa
zimeanza tena nchini Afghanistan ikiwa hatua muhimu kwenye juhudi za Serikali
mpya ya Taliban kurejesha hali ya kawaida baada ya kuchukua madaraka mwezi
uliopita.
Ndege ya Shirika la Qatar iliondoka jana kuelekea
Doha ikiwa na abiria 113 wakiwemo Raia wa Ujerumani, Marekani, Canada na
Uingereza na nyingine ya pili imetua Kabul leo.
Msemaji wa Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani
Ned Price amethibitisha kuwa Raia 10 na Wakaazi 11 wa kudumu wa Nchi hiyo
walikuwemo kwenye ndege hiyo, Mjumbe maalum wa Qatar nchini Afghanistan, Mutlaq
bin Majed al-Qahtani, amesema safari hii ni ya kawaida na si sehemu ya kampeni
ya kuwahamisha watu wanaotaka kuikimbia Afghanistan.
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Qatar, Sheikh
Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani amewashukuru Viongozi wa Taliban kwa kusaidia
kwenye kuufungua tena uwanja mkubwa wa ndege wa Kabul. #MillardAyoUPDATES

Post a Comment