POLEPOLE AHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI CCM, AKATAA KUSEMA KILICHOJIRI KIKAONI

MBUNGE wa kuteuliwa na Rais, Humprey
Polepole leo alifika mbele ya Kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM, akiitika
wito pamoja na wenzake Jerry Silaa na Josephat Gwajima ambao Bunge lilipitisha
azimio la kuwasimamisha kwa mikutano miwili kutokana na tuhuma za kusema uongo
na kushusha hadhi na heshima ya Bunge, mahojiano yanafanyika leo Dodoma.
Baada ya kumaliza mahojiano hayo, mbunge huyo ambaye aliwahi
kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, alitoka na kukutana na waandishi
wa habari ambao walipomuuliza nini kimejiri, alijibu.. "Utaratibu wa chama
chetu kikao cha maadili ni kikao cha ndani, kwa hiyo taarifa zote zitatoka kwa
utaratibu wa Chama”

Post a Comment