MUME WA NICKI MINAJ HATIHATI 'KUPIGWA' 10 JELA

MUME wa rapa Nicki Minaj, Kenneth 'Zoo
Petty '43' amekiri kufanya kosa la kushindwa kujiandikisha kama mtu aliyewahi
kufanya makosa ya Ukatili wa kijinsia alivyoanza kuishi katika jimbo la
California kama sheria inavyomtaka afanye.
Baada ya kukiri kosa, Kenneth sasa anasubiri ombi lake
kukubaliwa na mahakama huku wakiangalia adhabu atakayotajiwa mnamo Jan 24 2022.
Imeripotiwa anaweza kupewa kifungo cha miaka 10 na kuwa chini ya uangalizi katika
maisha yake yote.
Kesi hii inatokana na kosa alilofanya mwaka 1995 la kujaribu
kumbaka binti mwenye umri wa miaka 16, alitumikia kifungo cha miaka minne jela
na kutoka kwa masharti makali kama kutoa taarifa kwa mamlaka husika kila
anapohama jimbo lolote nchini Marekani. Kenneth na Nicki Minaj wana mtoto mmoja
ktk ndoa yao.

Post a Comment