KOREA KASKAZINI YAFANYA GWARIDE LA MIAKA 73 BILA KUONYESHA SILAHA

 North Korea stages midnight military parade in Pyongyang featuring hazmat  suits, gas masks | The Independent

TOFAUTI na ilivyo kawaida, Korea Kaskazini imefanya maonesho ya gwaride la kuadhimisha miaka 73 tangu kuasisiwa kwa taifa hilo, lakini haikuonyesha silaha.

Kinyume na ilivyo kawaida jeshi la taifa halikuonesha makombora yake ya masafa marefu mara hii. Aidha hakukuwa na mbwa wa ulinzi au wale wa kuwinda wala vifaru vya kijeshi.


Badala yake wanajeshi walivalia magwanda ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya maradhi yanayosambaa kwa hewa kama yale yanayotumika katika wadi za wagonjwa wa Covid19 ila zote zilikuwa za rangi ya chungwa.

Rais Kim Jong-un alihudhuria sherehe hizo, lakini hakuzungumza kama kawaida yake huku akionekana kuwa amepoteza uzani.

Wachambuzi wa siasa wanasema serikali ya Korea Kaskazini inataka kuonesha dunia kwamba juhudi zake kwa sasa zimeelekezwa zaidi katika masuala ya ndani ya nchi.


No comments