MAHUDHURIO YA WALIMU SASA KUHAKIKIWA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA

 Waziri Ummy Mwalimu awataka Walimu Wakuu kutoalika wageni rasmi wasio na  maadili mashuleni | MUUNGWANA BLOG

WAZIRI wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amesema Serikali inakusudia kuandaa mfumo wa kielektoniki wa alama za vidole kwa ajili ya kuhakiki mahudhurio ya Walimu kwenye shule mbalimbali za Tanzania.

Ummy amesema mpango huo ni kwa Shule zote za Msingi na Sekondari katika Halmashauri zote nchini ili kudhibiti mahudhurio ya Walimu Mashuleni, ametoa kauli hii wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Tawi la Tume ya Utumishi wa Walimu Dodoma. 

 

No comments