MBOWE, WENZAKE WATATU WAWASILI MAHAKAMA KUU KWA KESI YAO LEO

 Baada ya siku 14, Mbowe, Matiko warudishwa Mahakamani (+video) – Millard  Ayo TV

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu, wamewasili Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo kuendelea kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Mbowe na wenzake wanatakiwa kuwa mahakamani hapo leo baada ya kesi yao kusimama kwa siku nne kutokana na Jaji Elinaza Luvanda kujitoa kuisikiliza. Jaji huyo alijitoa Jumatatu baada ya washtakiwa kutokuwa na imani naye kwamba hawaamini kama atawatendea haki baada ya kutupilia mbali mapingamizi waliyoweka.

Mahakama sasa imemteua Jaji Mustapha Siyani kusikiliza kesi hiyo. Kwa mujibu wa hati ya wito, kesi itaendelea leo mahakamani hapo.

No comments