BEKI WA ZAMANI BAYERN ANUSURIKA JELA MIAKA MITANO, ALIMWA FAINI BILIONI 4

 Ex-Manchester City star Jerome Boateng fined £1.5 MILLION after being convicted of

JEROME Boateng, beki wa zamani wa Klabu za Man City, Bayern Munich na Ujerumani, amenusurika kifungo cha miaka mitano jela, lakini amelazimika kulipa faini ya paundi milioni 1.5, sawa na bilioni nne na ushee kwa fedha za Tanzania kwa kosa la kumpiga na kumsababishia maumivu mzazi mwenzake.

Boateng, 33, anadaiwa kumfanyia vitendo hivyo mchumba wake wa zamani, Sherin Senler wakiwa katika visiwa vya Caribbean mapumzikoni miaka mitatu iliyopita.

Senler, mama wa watoto wawili mapacha, aliiambia mahakama kwamba alipigwa usoni hadi damu kutoka na kubanwa kifuani kiasi cha kushindwa kupumua.

Boetang alikataa tuhuma zote na kudai kuwa ni yeye ndiye aliyekuwa akinyanyasika katika uhusiano wao.

731


 

No comments