MAAJABU HAYAISHI DUNIANI: MWANAMKE APATA PRESHA NA KUFA KUONA MKUSANYIKO MSIBANI KWAKE!

HAYA ni maajabu na kamwe
hayataisha duniani.
Huko Urusi, daktari aliyekuwa
akimtibu mwanamke aitwaye Fagilyu Mukhametzyanov alifanya makosa ya kitabibu na
kujikuta akithibitisha kifo cha mgonjwa huyo ili hali alikuwa bado hai.
Ndugu, jamaa na marafiki waliandaa msiba na shughuli ikafanyika nyumbani kwake. Mwili wake uliandaliwa tayari kwa ajili ya mazishi.
Siku ya kuzika akiwa kwenye
Jeneza alipata fahamu na kushangaa kukuta umati nyumbani kwao, ndugu, Jamaa na
Marafiki wakilia kwa uchungu. Alipouliza akaambiwa wanajua sababu waliambiwa
yeye amefariki, hapohapo presha ikapanda kwa mshtuko na akafariki kweli.

Post a Comment