JOE BIDEN, XI JINPING WAONGEA BAADA YA MIEZI SABA

RAIS wa Marekani Joe Biden
alizungumza na Rais Xi Jinping wa China jana jioni kwa mara ya kwanza ndani ya
kipindi cha miezi saba, wakijaribu kuuepusha ushindani uliopo baina yao kugeuka
kuwa mgogoro.
Viongozi hao wawili walikuwa na majadiliano mapana na ya
kimkakati ambapo walijadili maeneo ambayo masilahi yao hukutana, na maeneo
ambayo masilahi yao, maadili na mitazamo yao hutofautiana.
Ikulu ya Marekani, White House, ilisema kwenye mazungumzo
hayo kwa njia ya simu, ujumbe wa Biden ulikuwa ni kwamba Marekani inataka
kuhakikisha ushindani baina ya mataifa hayo makubwa duniani unasalia kwenye
kiwango ambacho hakutakuwa na hali yoyote ya kuwaingiza kwenye mgogoro
usiokusudiwa.
Mazungumzo hayo ni ya kwanza baina ya viongozi hao tangu
mwezi Februari, walipozungumza kwa masaa mawili muda mfupi baada ya rais Joe
Biden kumrithi Donald Trump

Post a Comment