MUIGIZAJI APIGWA FAINI BILIONI 105 CHINA, MARUFUKU KUIGIZA TENA

CHINA si mchezo. Muigizaji nyota nchini
CXhina amepigwa faini ya yuan ambazo ni fedha za chini kiasi cha milioni 299,
sawa na dola za Marekani milioni 46, ambazo kwa fedha za madafu ni zaidi ya
bilioni 105 kwa kukwepa kodi.
Mamlaka zimempiga faini Zheng Shuang kwa
ukwepaji kodi na kutotangaza kipato alichoingiza kutokana na kazi zake katui ya
mwaka 2019 na 2020 wakati amekuwa akiigiza tamthiliya mbalimbali.
Zheng, 30, alijipatia umaarufu mkubwa
nchini China baada ya kucheza kazi kali mwaka 2009 iitwayo Meteor Shower. Licha
ya faini hiyo kubwa, pia mamlaka zimewakataza maprodyuza wote nchini humo
kutompa tena kazi muigizaji huyo.

Post a Comment