MLIPUKO MWINGINE WATOKEA KABUL

 Watu kadhaa wajeruhiwa katika mlipuko nje ya uwanja wa ndege Kabul

 

Ripoti kutoka Kabul Afghanistan leo jioni zinasema umetokea mlipuko nje ya uwanja wa ndege wa Kabul ambako maelfu ya watu wamekusanyika kujaribu kuikimbia nchi hiyo kwa kutumia ndege za mataifa ya Magharibi tangu Taliban wachukue nchi mwezi huu.

Msemaji wa Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon John Kirby amethibitisha taarifa za mlipuko huo lakini madhara ya mlipuko huo bado hayajafahamika ila limetajwa kuwa ni shambulio la kujitoa muhanga.

Mataifa ya magharibi yalikuwa tayari yameonya juu ya uwezekano wa shambulio katika uwanja wa ndege wa Kabul saa kadhaa zilizopita wakihusisha shambulio hilo na kundi la Afghanistan lenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS ambalo uwezekano wa kufanya shambulio hilo umetokana na Taliban kuwaachia huru Wafungwa wengi ambao miongoni mwao wamo wa wa kundi hilo.

 

No comments