MANARA KAPATIA, YANGA WAMECHEMKA
Ni stori kila kona kuhusu ishu ya Haji Manara kutoka Simba kwenda Yanga. Yes, yeye si mtu wa kwanza kuhama upande, iwe kwa wachezaji, viongozi na hata makocha. Katika jambo hili la majuzi, kwa jicho la mbali kuna mambo ya kuyatupia.
Haji kakasirika kuondoka Simba. Ukiwa na kumbukumbu nzuri, ukarudia press conference kadhaa, unagundua kuwa siku zote hakuwa salama katika nafasi yake. Aliamini kuna watu hawamtaki, wanamuonea wivu na wanaitaka nafasi yake.
Haji aliamini kwa hamasa anayotoa, anastahili kubakia hapo kwa muda wote, asikumbuke kuwa kuna watu wengi wamewahi kuhudumu katika hiyo nafasi na kuondoka.
Haji ni mtoto wa mjini. Kuna watu wanaamini mafanikio ya Simba ameyaleta yeye na ndiyo maana kauli yake ya kwanza tu akiwa Yanga ni kuwaletea kombe. Hahahahahahahaaaaa.
Ukweli ambao Haji na wengine wanaukataa kuukubali ni kuwa klabu ya Simba ndiyo iliyompa umaarufu Haji na siyo kinyume chake. Ubora wa Simba uwanjani ndiyo uliompa jeuri Haji ya kuzungumza aliyokuwa akizungumza.
Simba haikucheza soka safi kwa sababu ya mdomo wa Haji ila Haji alipata nafasi ya kuchonga sana kwa sababu ya ubora wa Simba uwanjani.
Kwa kitendo hiki cha Haji kwenda Yanga, kwake ni sahihi kwa sababu nyingi, ikiwemo maisha, lakini kwa klabu ya Yanga, imechemnka big time.
Viongozi ni wazi walikuwa wakiumizwa sana na Haji akiwa upande wa pili, wakaacha kupambana kuijenga timu, wakaamini katika maneno ya Haji, ndiyo sababu ya kumleta Antonio Nugas, aje azungumze kama Haji.
Yanga kama timu, hawana umuhimu wowote na Haji. Ni tofauti na ilivyokuwa kwa Senzo. Hakuna thamani yoyote kwa klabu itaongezwa na Haji zaidi ya tambo za mashabiki.
Mahitaji ya mashabiki wa Yanga ni mafanikio uwanjani ambayo yataletwa na ushirikiano wa pamoja baina ya wadau wote wa klabu, wachezaji, benchi la ufundi nk.

Post a Comment