MAGORI AIZUNGUMZIA SIMBA, MO

MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba,
Crescentius Magori akiongea na Simba App jana, amezungumzia masuala kadha ya
klabu ya Simba sc juu ya Kambi, Usajili pamoja na maendeleo kiujumla.
1.Kuhusu Kambi.
Magori amesema kuwa klabu ya Simba sc
imefanikiwa kuweka kambi ya siku 14 yenye mafanikio makubwa , kwani kambi
ilikuwa na kila kitu kuanzia Gym mpaka viwanja vya mazoezi vye hadhi kubwa, kwa
Mujibu wa Magori amesema kuwa timu ilifikia kwenye hoteli ya Nyota 5 na
walikuwa wanafanya mazoezi kwenye viwanja bora kabisa ambavyo ni vya Mohamed wa
VI ambavyo timu yoyote Duniani inaweza kuvitumia.
Ameendele kusema kuwa kwa mujibu wa
Ratiba Simba sc imehitimisha kambi hii leo na muda wowote wataondoka kurejea
Tanzania kwa ajili ya kambi nyingine kwa ajili ya kuzoea Mazingira ya Afrika
Mashariki kwa wachezaji wao wapya.Pia amesema kuwa Wanafurahi kucheza michezo
miwili migumu kwa sababu FA Rabaat na Olympiques ni timu za daraja la Juu
Nchini Morocco.
Kuhusu USAJILI.
Magori amesema kuwa Simba sc imesajili
Vijana wenye njaa kubwa , wanaviwango Vikubwa sana, Magori amewasifia wachezaji
Wote waliosajiliwa akieleza sifa zao .Amesema kuwa Sakho ana attibutes zote za
King Kibadeni ni winga wa kisasa mwenye kasi nguvu na akili kubwa njee ya 18 ,
amemsifia pia Heneck Inonga beki toka DC Motemapembe beki ambaye anacheza miguu
yote miwili huku akiwa na utulivu mkubwa sana.Amemuelezea Peter Banda kuwa ni
hatari sana hasa kutokana na Spidi yake , feints , Agility na uwezo mkubwa wa
kufanya maamuzi sahihi ndani ya 18 huku akimuelezea Dancani Nyoni Kama mchezaji
anayekuja kuleta radha tofauti kutokana na uwezo wake wa kupiga kwa kushitukiza
eneo lolote huku akitumia mguu wa kushoto kama silaha.
Kuhusu Maendeleo
Magori amesema kuwa , Jana wamezindua
Simba APP kama sehemu ya mpango mkakati wa klabu kidigitali , amesema mpaka
jana Tsh 15M zilikuwa tayali zimekusanywa kupitia APP tu huku akiwaomba
wanasimba kupakuwa APP hiyo kwa ajili ya Exclusive interviews.
Ameendelea
kusema kuwa anashanga watu kumsema Vibaya Mo Dewji kuhusu kuposti vitu vya
Simba sc , amesema kuwa kikatiba Mo Dewji ni kiongozi wa Simba sc hivyo anahaki
yakufanya hivyo halafu Mo ni mshabiki wa Simba sc tangu akiwa mdogo so haiwezi
kuwa ajabu.

Post a Comment