GOLIKIPA PETER SHILTON AELEZEA ALIVYOATHIRIKA KWA KAMARI

]

PETER SHILTON: I couldn't save myself from gambling away my millions

MLINDA mlango nyota wa zamani wa England, ambaye ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi za timu ya taifa hilo, Peter Shilton, amezungumzia tabia yake ya kucheza kamari ambayo imemfanya kupoteza mamilioni ya shilingi.

Katika mahojiano maalum na gazeti la Daily Mail, mwanasoka huyo ambaye alimshukuru mwanamke mpya aliyempata ambaye aliweza kumponya maradhi hayo, amesema anafikiri amepoteza kiasi cha kama paundi za Uingereza laki nane (sawa na shilingi za kitanzania bilioni 2.4) katika kipindi chote alichocheza kamari yaani betting.

"Betting ni ugonjwa mbaya, ukianza kuumwa huwezi kuacha. Ni addiction kama addictions zingine," anasema Shilton, ambaye alikuwepo langoni wakati marehemu Diego Maradona akifunga bao maarufu la Mkono wa Mungu nchini Mexico mwaka 1986 wakati wa fainali za kombe la dunia.



No comments