WAZIRI ASHAMBULIWA, BINTIYE, DEREVA WAFA


Jenerali Katumba wa Uganda anusurika shambulio la mauaji | Matukio ya  Afrika | DW | 01.06.2021

HALI ya usalama inaonekana kuendelea kuwa tete nchini Uganda baada ya msafara wa Waziri wa Ujenzi, Jenerali Katumba Wamala kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana karibu na nyumbani kwake Mjini Kampala.

Mtoto wake, Brenda Wamala Nantongo na Dereva, Haruna Kayondo, wameripotiwa kupoteza maisha kufuatia tukio hilo. Mashuhuda wamesema walioshambulia walikuwa kwenye pikipiki.

Jenerali Wamala alikuwa Mkuu wa Jeshi la UPDF mwaka 2013 hadi 2017 baadaye akapewa Cheo cha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.

No comments