MAMBO YAMKALIA VIBAYA OLE SABAYA

Anaandika Malisa GJ
MOJA kati ya tuhuma
zinazomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ni unyanyasaji
wa kingono. Sabaya anadaiwa kulazimisha ngono wanawake mbalimbali, kuwachukua
kwa nguvu anapokutana nao kwenye klabu za usiku, na kuwapeleka hotelini kufanya
nao ngono kwa lazima. Jumla ya wanawake 40 wamejitokeza kutoa ushahidi
TAKUKURU.
Kati ya wanawake hao wapo
wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika mikoa ya Arusha na
Kilimnjaro. Kati ya wanafunzi hao wawili wanadai kulawitiwa baada ya kutekwa na
walinzi wa Sabaya walipokutana nae night club. Mmoja kati ya walinzi amekiri
kuwapeleka wasichana hao kwa Sabaya lakini amekanusha tuhuma za ulawiti.
"Tuliagizwa kuwachukua
lakini sikujua mahusiano yao na Mhe.Sabaya wala sikujua kama walikubaliana
kukutana. Nakiri kuwapeleka kwake lakini kuhusu kulawiti siwezi kutoa ushahidi
maana sikuwa naye ndani" mmoja wa walinzi wa Sabaya ameieleza timu maalumu
(task force) inayochunguza suala hilo kwa kushirikiana na TAKUKURU.
Sabaya anadaiwa kufanya vitendo
hivyo katika hoteli mbalimbali za kifahari jijini Arusha na amekuwa akiondoka
bila kulipa. Baadhi ya hoteli zimekiri kumdai Sabaya baada ya kupata huduma
mbalimbali ikiwemo malazi na chakula lakini amekua akindoka bila kulipa. CG
Hotel wanamdai 8.7M, Grand Melia 14.8M, Melvis Hotel 3.4M, na Massai Land 9M.
Sabaya ambaye yupo mahabusu
tangu May 25 mwaka huu, anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote ikiwa
ataonekana anazo tuhuma za kujibu.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP
Salum Hamduni jana alisema "Ni kweli tunamshikilia tangu jumanne ya wiki
iliyopita kwa mahojiano ya tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka na
rushwa. Akionekana ana kesi ya kujibu atafikishwa mahakamani"

Post a Comment