MTANDAO WA WANAOIBA MAFUTA WABAINIKA

WABONGO BWANA! Ukaguzi uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya
Kigamboni umebaini nyumba moja iliyopo Ulongozi ina vifaa vya kuchimba visima,
lakini vinatumika kuchimba kuelekea Bomba la Mafuta.
Katika Ukaguzi huo vifaa mbalimbali vimegundulika yakiwemo
magari yanayosadikiwa kutumika kubeba mafuta kutoka eneo wanalochimbia na
kuyasambaza maeneo mbalimbali jijini Dar.
Nyumba inayotumika kufanya shughuli hizo imekutwa na ulinzi
mkubwa wa Kamera na walinzi japo hapakuwa na shughuli yoyote inayoendelea
ndani. Imeelezwa, aliyepanga nyumba analipa Tsh. Milioni 60 kwa mwaka kama Kodi.

Post a Comment