WANANCHI WAMUWANIA BEKI WA KMC

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa katika hatua zake za mwishomwisho na dirisha la usajili likiwa bado kufunguliwa, zipo tetesi kuwa beki wa kushoto wa Kino Boys, David Brayson anatakiwa na wananchi, Yanga.
Beki huyo ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo ya Manispaa unaomalizika msimu huu, ni mmoja wa wachezaji walioitwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na amekuwa akiitwa tangu akiwa na kikosi cha Gwambina ya Misungwi mkoani Mwanza.
Inadaiwa kuwa Yanga ipo mwishoni
kumaliza dili hilo, ili Brayson aje kuja kuwa chaguo la kwanza katika nafasi ya
beki wa kushoto ambayo tangu ameondoka, Gadiel Michael hakuna aliyefiti kwa
uhakika.

Post a Comment