MARUFUKU KUUZA DAWA KWENYE MABASI


ITV Tanzania - #Habari:Chama cha wamiliki wa mabasi TABOA... | Facebook

SERIKALI imepiga marufuku tabia sugu ya baadhi ya watu kuuza dawa zinazotibu magonjwa mbalimbali kwenye vyombo vya usafiri, hasa mabasi ya mikoani na kuonya kuwa atakayebainika kuuza au kununua, atatozwa faini ya hadi milioni kumi.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba, Adam Fimbo, amesema ni marufuku abiria kununua dawa mbalimbali hasa za kutibu magonjwa zinazouzwa kwenye magari na vyombo vingine vya usafiri na kwamba endapo mnunuzi na muuzaji watakamatwa watachukuliwa sheria.

Mkurugenzi huyo amesema kabla ya kutumia dawa inapaswa mtu kupata ushauri wa wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kupata vipimo.

"Kwanza hilo haliruhusiwi kutangaza dawa kwenye vyombo vya usafiri, lazima upate ushauri wa daktari upime kwanza, natoa wito tena hairuhusiwi kuuza wala kununua,” alisisitiza Adam Fimbo

 

No comments