JUMA NYOSO ANAPITWA NA WAKATI


Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na nyasi

BAADA ya kupewa kadi ya pili ya njano na baadaye nyekundu kwa kumchezea faulo beki wa Simba, mashabiki wengi nchini wanasema nahodha wa Ruvu Shooting, Juma Nyoso anapitwa na wakati akiwa bado kijana.

Nyoso alimfuata na kumpiga kitu kama kofi beki Shomari Kapombe, wakati akienda kuufuata mpira uliotoka nje. Ingawa haikuonekana kama ni kitu kikubwa kwa Kapombe, beki huyo alilala chini kuonyesha kuumia na mwamuzi akampa Nyoso kadi ya njano, ikiwa ni ya pili katika mchezo huo kabla ya kumpa nyekundu itakayomfanya kukaa nje mechi mbili kati ya nne ambazo timu yake imebakiza.

"Nyoso mshamba, anacheza mpira wa kizamani katika mazingira ya kisasa. Wachezaji kama hao watajiondoa wenyewe," anasema shabiki wa soka John David akiiambia Ojuku Blog.

"Michezo kama hiyo wanachezaga watu wenye vipaji, siyo mtu butua butua kama Nyoso, mimi ningekuwa kiongozi wa Ruvu Shooting hiyo ndiyo ingekuwa mechi yake ya mwisho," anasema shabiki mwingine, Nasri Inno.

 

No comments