WANAFUNZI CHUO KIKUU WANYONGANA, KISA WIVU WA MAPENZI


JESHI LA POLISI IRINGA WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA SIKUU YA KRISMASS, MWAKA  MPYA - MICHUZI BLOG

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amethibitisha kuwa Petronel Mwanishawa mwenye umri wa miaka 22, ameuawa kwa kunyongwa na mpenzi wake, kisa ikidaiwa wivu wa kimapenzi.

Marehemu huyo aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Iringa, anadaiwa kunyongwa na mpenzi wake, Prudence Patrick (21), ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho.

Kamanda Bwire amesema tukio hilo limetokea Juni 1, mwaka huu maeneo ya Kihesa. Alisema siku ya tukio marehemu hakurudi nyumbani kwao jambo ambalo si kawaida yake, hivyo wazazi wake waliingiwa na hofu na kuanza kumtafuta.


"Marehemu alikuwa anaishi na wazazi wake, na huyu mtuhumiwa yeye alikuwa amepanga. Kwa hiyo siku ya tukio alitoka kwenda chuo, lakini mpaka usiku akawa hajarudi, ndipo wazazi walianza kupata wasiwasi, wakampigia simu rafiki yake lakini hawakufanikiwa," amesema Kamanda Bwire na kuongeza;

"Kwa hiyo jana ndo tukampata, na hiyo ni baada ya mtuhumiwa mwenyewe kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa mzazi wa marehemu akisema alikuwa na Petronel na kwamba amefariki. Baada ya hapo hakupatikana tena," alisema.

Amesema baada ya wazazi kupata taarifa hizo waliripoti kituo cha polisi, ndipo askari walikwenda katika nyumba ya mtuhumiwa na kuukuta mwili wa marehemu.
Bwire amefafanua kuwa, taarifa za awali zinaonyesha binti huyo alinyongwa na mpenzi wake na chanzo ni wivu wa mapenzi.
"Mtuhumiwa tulimkamata njia ya kuelekea Dodoma alipokuwa akijaribu kutoroka na upelelezi wa tukio hilo unaendelea," amesema Kamanda Bwire.

Credit: Mwananchi

No comments