SERIKALI YAKIRI KUSAFIRISHWA MAKINIKIA NJE YA NCHI

BAADA ya taarifa na picha zinazoonesha mchanga wenye madini maarufu kama Makinikia yakisafirishwa kuelekea bandarini Dar es Salaam kisha nje nchi, Waziri Mkuu ameibuka na kuweka wazi kuwa ni kweli Makinikia yanasafirishwa nje ya nchi.
Kauli hiyo ameitoa Bungeni leo Juni 3, 2021, wakati akijibu swali la Mbunge wa Msalala, Mhe. Iddi Kassim Iddi, aliyehoji kuhusu makontena ya makinikio ambayo yamekuwa yakionekana katika njia ya Bulynhulu Kahama na bandari ya Dar es Salaam yakisafirishwa kupelekwa nje ya nchi ili hali serikali mwaka 2018 ilizuia usafirishaji wa makinikia hayo.
"Na mimi pia nimeona kwenye mitandao kwamba watu wanaona makontena ya makinikia yakisafirishwa kwenda nje, niwatoe hofu Watanzania hayo wanayoyaona yameshauzwa na mnunuzi anakuwa huru kuyapeleka anapotaka, kwa hiyo waondoe mashaka hakuna kontena linalotoka nchini bila kuuzwa," ameeleza Waziri Mkuu Majaliwa wakati akijibu swali hilo.
"Na mimi nimeona pia kwenye
mitandao, watu wakionesha kwamba wanaona makontena ya makinikia, yakisafirishwa
kwenda nje...nataka niwaondolee hofu kwamba makontena hayo yameshauzwa tayari
na huyo ni mnunuzi, kwa hiyo waondoe mashaka juu ya usafirishaji wa makontena
hayo yenye makinikia, serikali iko makini" ameongeza Majaliwa.

Post a Comment