ISMAIL ISSA MICHUZI AFARIKI DUNIA DAR ES SALAAM

MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Ismail Issa Michuzi amefariki dunia asubuhi hii katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar alikokuwa akitibiwa maradhi ya tumbo.
Ismail, ambaye ni kaka yake mpiga picha maarufu na blogger
Muhidin Issa Michuzi, amefariki akiwa na umri wa miaka 61.
Ismail atakumbukwa kuwa mmoja wa viongozi na waanzilishi wa
bendi ya Dar International chini ya Marijani Rajabu na pia alihudumu kama
katibu wa bendi toka mwanzo wake hadi mwisho.
Baada ya Dar International kudumaa, Ismail alijiunga na Jeshi
na kuingizwa katika bendi ya Mwenge Jazz kama mpuliza trumpet. Alitumikia jeshi
hadi alipostaafu takriban miaka sita iliyopita na kuhamia Tukuyu Mbeya ambako
alifanya kazi kwa
Muda na Radio Chai Fm.
Mipango ya mazishi inafanyika Tabata Mawenzi, Dar. Taarifa
kamili za maziko zitatolewa baadaye.

Post a Comment