TUNDU LISSU ATAKA SABAYA ATENDEWE HAKI

MWANASHERIA maarufu nchini, ambaye pia alikuwa mgombea wa Urais wa uchaguzi uliopita kupitia upinzani, Tundu Lissu, ametaka haki kutendeka katika kushughulikia suala la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya.
Sabaya anashikiliwa
na vyombo vya dola akihojiwa kwa tuhuma kadhaa zinazomkabili, akiwa mikononi
kwa zaidi ya wiki moja iliyopita.
Katika akaunti yake
kwenye mtandao wa Twitter, Lisu anayeishi uhamishoni Ubelgiji, alisema pamoja
na mabaya yote yanayosemwa juu ya Sabaya, kitendo cha kushikiliwa bila
kufikishwa mahakamani ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
"Kumuweka
ndani kwa wiki nzima ni kukiuka sheria zetu na kuendeleza tabia ya ukiukwaji wa
haki za binadamu wa vyombo vyetu vya usalama."

Post a Comment