MBRAZIL WA SIMBA APONA MAJERAHA, YUPO TAYARI KUREJEA

  

KIUNGO kisiki raia wa Brazil, Gerson Fraga wa Simba SC Tanzania amepona majeraha na yupo tayari kurudi dimbani, Fraga aliondoka nchini na kurudi kwao Brazil kuuguza majeraha kwa makubaliano maalumu ya pande zote mbili mwaka jana 2020.

Fraga amepona majeraha yake wakati mkataba wake ukiwa ukingoni, mkataba wa Fraga kuitumikia klabu ya Simba unafika tamati June 30, 2021.

Klabu ya Simba bado haijaweka wazi kama watamuongeza mkataba mpya baada ya mkataba wake wa sasa kufika tamati au wataamua kuachana nae.

Kwa upande mwingine hii sio habari nzuri kwa kiungo wa Simba Mtanzania Jonas Gerald Mkude, Mkude ambaye mara kwa mara amekuwa akituhumiwa kwa utovu wa nidhamu anacheza namba moja na Fraga pamoja na Taddeo Lwanga hivyo kurejea kwa Fraga kutafanya nafasi hiyo iwe na wachezaji wa uhakika zaidi ya mmoja jambo ambalo linaweza kusababisha Mkude aendelee kuwa na nafasi finyu zaidi kuliko hivi sasa na pengine hata kuruhusiwa akatafute changamoto mpya katika klabu nyingine .

 

No comments