ALIYESIMAMISHWA AREJESHWA YANGA
WAKILI Simon Patrick, ambaye alisimamishwa na Klabu yake ya Yanga katika nafasi ya Ukurugenzi wa Sheria na Wanachama amerejeshwa kufuatia Kamati Huru iliyoundwa kuchunguza tuhuma dhidi yake, kutobaini lolote.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo
usiku wa jana, imesema Kamati huru iliyoongozwa na Wakili Raymond Wawa,
haikubaini lolote katika tuhuma zilizoelekezwa kwa Simon na hivyo baada ya
kujadiliana kwa kina, Kamati ya Utendaji imejiridhisha pasi na shaka kwamba
Wakili Simon Patrick hakuwa na hatia katika tuhuma zilizopelekea kusimamishwa
kazi Novemba 18 mwaka jana.

Post a Comment