TANZANIA RAIS MPYA MAHAKAMA YA AFRIKA


Jaji Imani Aboud Apendekezwa Kugombea Urais Wa Mahakama Ya Afrika

JAJI wa Mahakam Kuu ya Tanzania Imani Daud Aboud amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu akichukua nafasi ya Jaji Silvian Ore kutoka Ivory Coast ambaye amemaliza muda wake.

Jaji Imani ameibuka Mshindi katika kinyang'anyiro kilichowahusisha Wagombea Wanne ambao wote ni Wanawake kutoka Mataifa ya Cameroon, Malawi na Nigeria.

Hii ni Mara ya Pili Kwa Mwanamke kushika wadhifa huo ambao uliwahi kushikwa na Sophia Akufo Mwanamama kutoka Nchini Ghana.

Hii ni mara ya Pili katika Historia ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa Mtanzania kushika wadhifa huo wa juu ambapo awali Marehemu Jaji Augustine Ramadhani aliyehudumu kwenye nafasi hiyo kati ya Mwaka 2014-2016.

Nchi 31 kati 55 za Afrika ziliridhia itifaki ya uanzishwaji wa Mahakama hiyo mbapo Tisa kati ya hizo zilitoa tamko la kuridhia Wananchi wake kupeleka Mashkata mbele ya chombo hicho.

Kwa hivi sasa nchi nne ambazo ni Tanzania, Rwanda, Benin na Ivory Coast zimeandaa tamko la kuruhusu wananchi wake pamoja na asasi za kiraia kupeleka mashauri kwenye mahakama hiyo.

Jaji Imani Aboud akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi anasema mpango wake mkubwa ni kuhakikisha nchi hizo zilizojitoa zinarejea pamoja na kuhimiza ongezeko la wanachama wapya.

Kabla ya uchaguzi wa rais limeshihudiwa zoezi la kuwaapisha majaji wawili ambao ni Dumisa Ntsebeza kutoka Afrika Kusini na Sacko Modibo kutoka Mali.

Mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu na Watu ilianzishwa Mwaka 2006 Chini ya Umoja wa Afrika na kuanza kufanya kazi Addis Ababa Ethiopia kabla ya kuhamia kwenye Makao yake Makuu Jijini Arusha Nchini Tanzania Mwaka 2007.

No comments