STELLA MANYANYA AMTETEA ALIYEFUKUZWA BUNGENI


Mbunge Condester Michael atimuliwa Bungeni kwa kuvaa ovyo. Spika awaagiza  askari wa bunge kuwazuia getini | JamiiForums

BAADA ya Mbunge Condester kufukuzwa bungeni jana kwa madai ya kuvaa nguo zisizo na staha bungeni, mbunge wa Nyasa, Injinia Stella Manyanya ameamua kusimama na kumtetea;

"Jambo lililonifanya nizungumze mimi Mtu mzima leo ni kilichotokea leo asubuhi ilibidi nifuatilie kwa karibu sana kwenye mitandao, hivi hiyo nguo ilikuaje? hali halisi ikoje? baadae niliishia kusononeka, Vijana kama hawa sisi wenyewe tumesema waingie Bungeni lakini hatutegemei kijana aingie Bungeni amevaa gauni tulilokuwa tunalivaa sisi zamani”

“Vijana lazima wachukuliwe kwa ujana wao ili mradi hizo nguo wanazovaa ziwe na heshima yake, hata jana wakati tunapitisha bajeti ya Wizara ya Habari, Sanaa, Utakaduni na Michezo limezungumzwa jambo tena wakaenda mbali wakasema acheni Vijana wapige kiki zao lakini hii haikuwa kiki lilikuwa ni vazi nadhifu la kijana” 

“Sitegemei wote sisi tutavaa vitenge, sitegemei wote sisi tutaamka tutavaa dera kila Mtu na utamaduni wake ili mradi liwe vazi la heshima, labda pengine niseme kwamba kuomba radhi ni sawa lakini mimi ningeshauri kwa sababu ya mazingira ya kiutu uzima pengine na yeye aliyetoa hoja kwa sababu ya uzoefu wake alitegemea atuone wote tuko vile pengine sio lazima sana tukamuamsha atuombe radhi lakini la msingi tuone jambo lililotendeka leo sio la haki"

 

No comments