NATAKA SPIDI MRADI MWENDOKASI- RAIS SAMIA

RAIS Samia Suluhu Hassa amemtaka mkandarasi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka kuelekea Mbagala kuongeza kasi ya ujenzi wake, kwani amesisitiza ya sasa hairidhishi.
Akiwa katika eneo la Mbagala Zakhem
ambako alifanya ukaguzi wa mradi huo alisema;
“Nilikuwa napitia mafaili ya miradi ofisini nikauona mradi
huu wa mwendokasi Mbagala, mradi huu kwa sasa ulikuwa ufikie asilimia karibu 60
na kitu lakini kwa taarifa nilizopata leo mradi upo kwenye asilimia 16 tu,
nikasema tuje tuone kinachokwamisha mradi huu.
“Tumeongea na Wasimamizi wa mradi huu wa mwendokasi Mbagala
na pia Wakandarasi na tumeona kinachokwamisha mradi, Serikali bado
hatujaridhishwa na kasi yake ingawa mwishomwisho hapa wameongeza speed kidogo,
tumekubaliana waongeze kasi zaidi ili mradi umalizike
“Tunataka mradi huu wa mwendokasi Mbagala umalizike ili
kurahisisha safari zenu Wananchi na tuinue uchumi, Serikali juzijuzi hapa
tumembadilisha Kiongozi mkubwa wa mradi huu tumemuweka mwingine ili atusaidie
kuongeza kasi ya mradi huu”

Post a Comment