MANJI ADONDOKA BONGO AKITOKEA UGHAIBUNI


Yusuf Manji bado mwarobaini Yanga - Mwananchi

HABARI nzuri kwa wanamichezo na hasa mashabiki wa Klabu ya Yanga ni kwamba aliyewahi kuwa bosi wao, Yussuf Mehboob Manji ameingia nchini akitokea Ughaibuni alikoishi kwa muda kadhaa.

Mfanyabiashara huyo ambaye wakati akiwa bosi wa Jangwani, timu hiyo ilikuwa haifungiki na ilitwaa makombe yote, alipotua Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, anadaiwa kuhojiwa na maofisa wa Uhamiaji ili kujiridhisha na uraia wake.

 

No comments