SEY AFUNGUKIA USHANGILIAJI WA MORRISON

 

Inaweza kuwa picha ya Mtu 1, anacheza spoti, nyasi na maandishi

MSHAMBULIAJI mahiri wa Namungo FC, Mghana Stephen Sey akiongelea tukio la Bernard Morrison kushangilia kwa staili yake, ametumia msemo wa Kiingereza usemao, “What goes around comes around,” akiwa na maana kwamba kile ambacho alikuwa akikifanya pindi afungapo mabao kilimrudia kwenye mchezo huo wa kiporo.

“Bado safari inaendelea na hizi ni mbio ndefu, tulikuwa kwenye nafasi ya kuushinda mchezo lakini mambo yaligeuka na tukajikuta tukipoteza, nadhani uzoefu umewabeba Simba,” alisema.

Sey alimsifu rafikiye huyo wa karibu Morrison kwa bao lile akisema ni moja ya mabao bora kabisa msimu huu.

 

No comments