MECHI YA SIMBA VS YANGA JULAI 3 IPO HAIPO


Michezo Tz - HASSAN BUMBULI "Hii kesi ni ya YANGA na... | Facebook

MECHI ya mzunguko wa pili kati ya watani wa jadi wa soka nchini, Simba na Yanga, iliyopangwa kupigwa Julai 3 mwaka huu, haina uhakika wa kuwepo kutokana na viongozi wa Jangwani kuanza kuleta hofu.

Msemaji wa Yanga, Hassan Bumbuli amesikika akiiambia redio moja ya mtandaoni kuwa wao wamebakiza mechi nne ili kumaliza Ligi Kuu na kati ya hizo, ile ya Simba hawaitambui.

Kauli hiyo imezua taharuki kiasi cha kupelekea Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo kutoa tahadhari kwa Yanga kuzingatia kanuni, lakini shaka zaidi imekuja baada ya Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, kwanza kuibuka na kuikana kauli ya Bumbuli, lakini akatia mashaka zaidi aliposema;

"Uongozi wa Yanga utatoa taarifa rasmi juu ya msimamo wake kuelekea mechi hiyo."

MECHI IPO AU HAIPO?

No comments