SABAYA HAYUPO PEKE YAKE, NAO WAKAMATWE


Lengai Ole Sabaya (@powersabaya) | Twitter

TAASISI ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa ikiwa inaendelea na mahojiano na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, wananchi toka pembe zote wametaka mamlaka kuwakamata na viongozi wengine ambao wanaamini walikuwa na tabia kama za mteule huyo wa Hayati John Magufuli.

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, wananchi hao wanadai tuhuma za rushwa, vitisho kwa wafanyabiashara, utekaji nyara, kutesa na maovu mengine anayotuhumiwa nayo Sabaya, yamefanywa na wateule wengi wa serikali ya awamu ya tano na kutaka nao wakamatwe.

Majina kadhaa yamekuwa yakitajwa yakiwahusisha viongozi hao, wakiwemo mawazili, wakuu wa mikoa na wilaya aingawa hata hivyo, jina la mkuu mmoja wa mkoa na mwingine wa wilaya, yamekuwa yakijirudia zaidi wakitakiwa kuchukuliwa na vyombo vya dola ili kuhojiwa na kufikishwa mahakamani.

No comments