HAMIS KIGWANGALAH ASHAMBULIWA MITANDAONI


Tanzania to become a Poaching Free Country by 2022” Government | WWF

 MBUNGE wa Nzega na ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala amekutana na wakati mgumu baada ya kupost katika akaunti yake mtandaoni akitaka watu kupendana na kutoombeana mabaya.

Aliandika hivi;

"Wakati unanishambulia, unanitukana, unanipiga vita, unanichukia, unapambana kunishusha na kuniangusha, unanipiga fitna na majungu nianguke, nipotee, jua tu unawatesa wanangu. Haunimalizi mimi tu. Hawa hawana makosa yoyote. #NasKigwa, The Duke of Igalula, is innocent na hana noma na mtu. Fikiri mara mbili kabla hujamshambulia mtu. Tupendane jamani. Spread the love!"

Baada ya post hiyo, wachangiaji wengi walimshushua, wakisema wakati akiwa waziri alifanya maovu mengi bila kujali wale aliowaumiza nao wana wazazi, watoto na watu wanaomtegemea.

No comments