RAY C AMNANGA DIAMOND, APULIZA

NYOTA mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ambaye pia anajulikana kama kiuno bila mfupa, amekataa kumumunya maneno. Amempa kavukavu Diamond Platnumz ambaye ni msanii pekee Afrika Mashariki anayewania tuzo za kimataifa za BET.
''Kuanzia leo nimeokoka..Anyway
kufupisha tu maneno...Tunachokizungumzia sasa ni uzalendo sio mtu binafsi! Na
Uzalendo unaanza kwako mwenyewe !!!Ok kwa kifupi tu Lile cheko lako la Pepsizo
la fiesta kwa kweli lilinikera sana hasa ukizingatia show ilikuwa ya wasanii
wenzio wa hapohapo Tanzania...(Ulikuwa sio uzalendo). Kuna kabati pale kwako
limejaa matuzo makubwa makubwa. Naamini Watanzania walichangia sana kujaza tuzo
kwenye lile kabati kwa upendo na kujibana matumizi! wengine kujinyima hata
chakula kuweka bando kuvote ututoe kimasomaso na kweli kwa upande wa kututoa
kimasomaso muziki wetu kuheshimika barani Africa hilo umeliweza asilimia 150!! Yanayoendelea
mitandaoni hasa twitter nadhani hata wewe huelewi mbona watu wameanza kuchange
ghafla wakati miaka kama mitano nyuma watu tulikuwa hatuskii wala hatuambiwi
kitu ni D D tu (mmoja wapo mimi) pitia posti za nyuma!!!!..nadhani hapo
katikati ulikuwa unatuchamba sana! kama vile I got money more than you
mazafantaz! (Sio Uzalendo)!!au zile interview za
madongo kusanya wasanii wote Tanzania wafanye show na mimi nifanye show tuone
nani atajaza.(Sio Uzalendo)? Kuna mda unakaa unajiuliza huyu dogo
mbona hivi tena !Bora hata saivi unatupa break kidogo unawachamba Forbes (ingawa
hata vile haipendezi kimataifa) Vichambo vyako vingi vimewagawanya mashabiki. Huo
ni ukweli. PLS kuwa humble sasa..Na pia punguza machawa wa ajabu wanaropoka
sana wanakera. Sema nini tunasonga mbele. Anza kufanya macolabo pia na wenzio
hapo Bongo.(Na simaanishi wasanii wa WCB tu). Wengine ambao
wanapambana na wanafanya vizuri kwenye Game!!!Washike mkono wenzio babaa
utapata baraka zaid sababu Uzalendo uanzie kwako pia sio kwenye team yako tu. Au
vipi babaa? Nitaendelea kusapotii yeyote
anaefanya poa na kwenye ukweli ntasema pia. Si ndio maana ya kuwa dada au? Mpaka BUNGE limetushawishi kukusapoti na ni kweli
tunakusapoti watanzania sasa basi tuendelee kubaki kwenye uzalendo huohuo kuwa
na wewe pia wainue wasanii wenzio wengine kwa kushirikiana nao waonekane Africa
ishangae na ione kuwa Tanzania kuna vipaji balaa! Anyway wabongo fanyeni kama
mnajikuna mkavote tuchukue na hii tuzo. GET THEM BRO diamond '' @rayctanzania

Post a Comment