RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHTUKIZA SOKONI KARIAKOO

RAIS Samia Suluhu
Hassan asubuhi ya leo ameshtukiza kuingia sokoni Kariakoo na kusikiliza kero
mbalimbali za wafanyabiashara.
Akiongea kwa kifupi
akiwa juu ya gari, mama Samia amesema amesikiliza kero zote kutoka kwa
wafanyabiashara, amejionea jinsi bidhaa zinavyokaa na ameshangazwa na mapato
yanavyopatikana na kutumika.
Akasema wakati
anaenda kukaa na wataalam ili kufanya tathmini, viongozi waliopo wakae pembeni
ili kupisha uchunguzi.

Post a Comment