MBUNGE ATOLEWA BUNGENI KWA MAVAZI YASIYO NA STAHA


Sichalwe.jpg

KANUNI bwana! Mbunge wa Momba, Condester Michael Sichalwe amejikuta pabaya baada ya kuamriwa kutoka bungeni mjini Dodoma kutokana na kuvaa mavazi yasiyo na staha na yasiyoruhusiwa kwenye kanuni za bunge.

Spika baada ya kumuamrisha kuondoka Bungeni pia aliwaambia askari wa Bunge, kuanzia sasa mbunge yeyote atakaevaa mavazi yasiyo na Staha na kinyume na kanuni waishie getini.

Sakata hilo lilianza kwa mbunge mwenzake kuomba muongozo wa spika akimtolea mfano kama mbunge aliyevaa mavazi yasiyo na staha.

No comments