RUVUMA KUPANDA MITI HEKTA 40,000 YA BIASHARA
NA STEPHANO MANGO, SONGEA
MKOA wa
Ruvuma umelenga kupanda miti ya biashara hekta 40,000 hadi kufikia mwaka 2025.
Mshauri
wa Maliasili Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe amesema mradi huo unatekelezwa
katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2015 na kwamba unatekelezwa kwa
kupanda miti maeneo ya serikali kuu, serikali za mitaa, vyuo, mashule na
vijiji.
Ameitaja
aina ya miti inayopandwa kuwa ni ile inayofaa kwa ajili ya malighafi za viwanda
vya mazao ya misitu ambayo ni misindano (pine),milingoti (Eucalyptus) na misaji
(Teak).
“Hadi
kufikia mwaka 2020 jumla ya miti ya biashara iliyopandwa na Wakala wa Huduma za
Misitu (TFS) misitu ni hekta 4,785, Halmashauri hekta 425, vyuo na mashule
hekta 420 na watu binafsi hekta 23,964, ambayo inafanya jumla ya mashamba yote
kuwa hekta 29,194 sawa na asilimia 56.1 ya lengo’’, alisema Challe.
Katika
hatua nyingine Mshauri huyo wa Maliasili, amesema Mkoa wa Ruvuma, unatekeleza
mradi wa kuongeza thamani mazao ya misitu na nyuki kwa kushirikiana na FORVAC
na kwamba mradi huo unatekelezwa katika wilaya zote tano za Mkoa huo.
Challe
amesisitiza kuwa mradi huo umelenga kuwezesha vijiji kutunza misitu ya hifadhi
ya vijiji na kuwawezesha kupata faida kutoka kwenye misitu hiyo na kwamba
wilaya za Tunduru na Songea zimepata mashine za kisasa kwa ajili ya kuchana
mbao ili kuongeza mbao thamani.

Post a Comment