CHALAMILA APIGWA CHINI MWANZA
RAIS Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, na kumhamishia mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Hatua hiyo imetokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya
mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine.
Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika mabadiliko hayo
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia amemteua Katibu Tawala
wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua
nafasi ya Ally Salum Hapi.
Aidha Katibu Twala Wilaya ya Simanjoro Zuwena Omari Jiri
ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda
Salha Buriani.
Taarifa hiyo imesema tarehe ya uapisho wa viongozi wapya
itatangazwa baadae.

Post a Comment