MNYAMA ATAMBA, RUVU HAWATOKI LEO

WAKATI itaendelea kumkosa kiungo wake mchezesha timu Clatous Chota Chama na beki kisiki Joash Onyango, mabingwa watetezi Simba wamejitapa kuwa kesho wataibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting ugenini CCM Kirumba jijini Mwanza.
Chama yupo nyumbani kwao Zambia alikofiwa na mkewe wakati Joash ni majeruhi.
Kocha msaidizi wa SimbaSuleiman
Matola ametabiri mechi kuwa ngumu hasa kwa vile awali walifungwa, lakini
akajipa matumaini kwamba wamejipanga kuondoka na alama zote tatu.
Nahodha msaidizi wa Simba Mohamed Hussein amesema kikosi kipo imara kuelekea mchezo wa kesho na Wana imani watachomoza na ushindi.
Kocha mkuu wa Ruvu Shooting
Charles Boniface Mkwasa Master anaamini rekodi nzuri iliyonayo timu yake dhidi
ya Simba itatumika kuamua mchezo wa hapo kesho.

Post a Comment