MANJI MIKONONI MWA TAKUKURU


Manji mgonjwa - Mwananchi

 SIKU moja tu baada ya kurejea nchini akitokea ughaibuni alikokwenda kwa muda wa miaka kadhaa, mfanyabiashara maarufu nchini, Yussuf Mehboob Manji, amefikia mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi toleo la leo Juni 3, 2021, inadaiwa tuhuma zinazomkabili ni tatu, zikiwemo ukwepaji kodi na fedha za Klabu ya Yanga ambayo alikuwa Mwenyekiti wake na mfadhili wake mkubwa.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Kamanda Hamduni alikiri kuwa walimkamata juzi uwanja wa ndege mara tu baada ya kutua na kwamba hawajui lini watamuachia, kwani hiyo itatokana na jinsi mahojiano yakatavyokuwa.

No comments