HAKUNA MBONGO ANAYEWEZA KUMFANYA DIAMOND ASHINDE/ASHINDWE BET

Yes, huo ndiyo ukweli. Kama ambavyo hakuna
Mtanzania yeyote aliyeshiriki mchakato wa kumfanya Diamond awe ndiye msanii
pekee kutoka Afrika Mashariki kuwania Tuzo hizo, ndivyo hivyo hivyo ambavyo
hakuna kura ya ushindi kutoka hapa.
Why? Nitajaribu kufafanua.
Katika kutafuta washindi wa kura kubwa kama
hizi, wapiga kura huwa ni wateule maalum ambao kwa kawaida, ni washirika wa
mtoa tuzo.
Nitatolea mfano wa hapa nyumbani. Nilikuwa mmoja
wa wapiga kura wa kuwachagua wasanii bora nyakati zile za Kili Music Awards.
Nilifanya hivyo mara mbili. Kulikuwa na kitu kinaitwa Academy, hili ni kundi la
washirika wa watoa tuzo ambao by then walikuwa ni Tanzania Breweries Ltd.
Academy ile ilijumuisha waandishi/watangazaji wa
habari za burudani (kigezo kilichoniingiza), wahusika wa muziki (BASATA) na
wadau. Wadau ni watu wote wenye influence katika tasnia, kwa muziki wetu
walijumuisha watu kama maproducers, DJs, mapromota na mtu mmoja mmoja ambaye
anaonekana kuwa mtu wa muziki. Katika moja ya hizo academy, Dotnata aliingia
kama mdau wakati huo hajaanza kuimba, alikuwa muigizaji tu.
Hii Academy ndiyo inafanya mchakato wote baada
ya wenye muziki, BASATA kutoa mwongozo wa nyimbo na video za namna gani
zinatakiwa kupigiwa kura, hawa wakisimamia zaidi maadili na maudhui.
Wataalam wa video wanaalikwa pia kuelezea nini
maana ya video bora, quality, jinsi maudhui yalivyoendana na locations na vitu
kama hivyo.
Katika Academy zote mbili za Kili Awards kwa
mfano, walisema sharti muhimu la wasanii watakaopigiwa kura ni wale waliotoa
nyimbo mpya mwaka huo.
So categories zikatolewa. Tukaanza kwanza kutaja
wasanii wengi kwa kila category, kisha tukawapigia kura ili kubakiza namba
iliyotakiwa, by then nafikiri ilikuwa wasanii watano kila category.
Mwisho, tukatakiwa kupiga kura za kuwachagua
washindi, lakini kwa maelezo kuwa kura zetu zitajumuishwa kwenye matokeo ya
mwisho ambayo majina ya wasanii shiriki yalitolewa kupitia vyombo vya habari na
mashabiki kutakiwa 'kupiga kura'.
Ile kusema mashabiki wanatakiwa kupiga kura ni
kuwaridhisha tu, maana wahusika ndiyo huamua kwa kuongozwa na kura za academy
nani apate nani akose. Ndiyo maana kila mwaka kulikuwa na lawama nyingi, baadhi
ya watu wakinyooshewa vidole kuwa ndiyo wanaopanga matokeo!
Mambo yako The Same kule BET. Wana Academy yao
na hao ndiyo waliofanya mchakato ambao umemuingiza huyu dogo. Wana vigezo
ambavyo Diamond ali-fit. Hii haimaanishi kuwa Mondi ni msanii mkali kupita wote
Afrika Mashariki na Kati, au labda Burna Boy na Wizkid ndiyo wababe sana
Nigeria, No, ni vigezo tu. Na siyo kweli pia kwamba eti Aya Nakamura
(France), Emicida (Brazil), Headie One (UK) Young T na Bugsey (UK) na Youssoupha
(France) ndo wakali sana huko kwao.
Kwa BET washirika wao kwa Afrika wanaweza kuwa
media house kubwa let say DStv na labda mawakala wao. Hawa wote walishiriki
katika academy na wao ndiyo wanajua nani mshindi.
Ni kama anavyopatikana mwanasoka bora wa dunia.
Dunia haipigi kura, isipokuwa makocha na manahodha wa timu za taifa pekee ndiyo
wapiga kura na mshindi huhesabika wa dunia nzima.
Lugha nzuri kwa mashabiki wa Diamond ni kusema
wanamuombea ushindi, that's all! Na kwa wale wanaosema hawatampigia kura, nao
ni vilevile, hawatabadili chochote, sana wanachojaribu kufanya ni kumtumia
ujumbe Diamond kwamba hawamuungi mkono kwa bifu zao.
To be honest, nitamuombea kama Mtanzania ashinde!

Post a Comment