MHANDISI ARUHUSU UJENZI MRADI WA MAJI YENYE CHUMVI

MHANDISI wa Maji wa Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) wilaya ya Hanang, Herbert Kijazi ameondolewa katika Wizara ya Maji baada ya kugundulika kuruhusu ujenzi wa mradi wa maji, licha ya ripoti ya maabara kuonyesha kuwa maji hayo yalikuwa na chumvi nyingi isiyofaa kwa matumizi ya binadamu.
Uamuzi huo uliifanya serikali kupata hasara ya shilingi
milioni 609 kutekeleza mradi huo.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametaka meneja wa Ruwasa mkoani Dodoma,
Godfrey Mbabaye na meneja wa Wilaya ya Kongwa, Kaitaba Rugakingira kujieleza
kwake kwa nini wasifukuzwe kazi kwa kutaka kusababisha hasara nyingine baada ya
kumweleza kuwa wanahitaji Sh360 milioni.
Mameneja hao awali walimweleza waziri huyo kuwa wanahitaji
kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kukarabati mradi huo.
Aweso alivyokwenda katika kijiji hicho na kuwasikiliza wakazi
wa eneo hilo walimweleza kuwa maji hayo yana chumvi na hayafai kwa matumizi
yoyote ya binadamu.
Kauli za wananchi hao zilimfanya Aweso aagize kupigiwa simu
kwa Kijazi na alipoulizwa kama ripoti ya maabara ilionyesha nini kabla ya
utekelezaji wa mradi huo, alijibu kuwa ilionyesha kuwa maji hayo yanafaa kwa
matumizi ya binadamu.
“Amesababisha hasara kwa Serikali, ujumbe umfikie katibu mkuu
( Anthony Sanga) kuwa huyu mhandisi hana kazi hapa wizarani,” amesema Aweso na
kuwafanya wakazi wa eneo hilo kushangilia.

Post a Comment