IRINE PAUL AMUITA DIAMOND NEMBO NA KINARA

HUKU Watanzania ambao ni mashabiki wa muziki wakigawanyika kuhusu nafasi ya Diamond Platnumz katika Tuzo za BET alizoteuliwa kuwania, muigizaji nyota wa filamu nchini, Irene Paul, ametaka ni wakati wa wananchi wote kuwa kitu kimoja kwa Tanzania.
Anasema: "TANZANIA
YETU.....LETS VOTE Ifike mahali tuthamini juhudi za mtu binafsi katika kuleta
heshima kwa taifa letu na tuache mengine yote pembeni, hebu tufikie stage
kukubali kwamba at the end of the day huyu ndio "NEMBO NA KINARA" ya
mziki wa Tanzania kwa sasa.
"Sikatai na wala sipingi kuwa kuna wengi wazuri zaidi
yake na kuna wanaofanya vizuri lakini haitatosha kumvua #platnumz heshima
aliyotuletea kama Tanzania pamoja na mengine yote yanayoendelea,WENGI WATAFUATA
LAKINI NI BAADA YA YEYE KUCHORA RAMANI YA JINSI INAVYOFANYIKA.
"Ninatamani tumpigie kura kwanza huko kwa #BET then turudi
nyumbani tuongee tunayojisikia maana at the end of the day tutakuwa
tumeshatambulika zaidi na kujulikana kama Tanzania. LETS VOTE and VOTE and VOTE
again....tupeperushe Tanzania yetu. N.B :jamani kwa wale wa ma team na maneno
machochezi post hii haiwahusu'' @irenepaul001

Post a Comment