MESSI AKARIBIA KUSAINI TENA BARCELONA


Barcelona president determined to convince Lionel Messi to stay | The Japan  Times

ARSENAL wanaongoza kwenye mbio za kumpata winga wa Manchester City Muingereza Raheem Sterling, 26, mpango ambao unaweza kumzuia mshambuliaji Harry Kane, 27, kujiunga na City akitokea Tottenham. (Sun)

Manchester United wanakabiliwa na ushindani katika kumnasa mlinzi wa Sevilla Jules Kounde kwani Barcelona pia ina mpango wa kumsajili mchezaji huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22. (Mundo Deportivo)

Arsenal wanajiandaa kukamilisha taratibu za kumsajili mlinda lango wa Cameroon Andre Onana, 25, kutoka Ajax, kwa pauni milioni 1.7 (Nos-in Dutch)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich binafsi ana mpango wa kumchukua mshambuliaji wa Ubelgiji anayekipiga Inter Milan Romelu Lukaku , 28, kumrejesha klabuni hapo. (Eurosport)

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, yuko karibu kukubali mkataba wa miaka miwili kusalia Barcelona. (AS-in Spanish)

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel atapatiwa mpaka pauni milioni 200 kwa ajili ya matumizi ya msimu huu wa kiangazi. (Metro)

Kiungo wa kati wa Barcelona Miralem Pjanic, 31, anataka kurejea Juventus. (Tuttosport)

Kocha mpya wa Roma Jose Mourinho anatazamia kumsajili mlinda mlango wa AC Milan, Muitaliano Gianluigi Donnarumma, 22. (Mirror)

Manchester United wanamtolea macho kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Pedro Goncalves, 22. (Record-via Star)

Leeds United itatafuta mbadala baada ya kushindwa bei ya kumpata beki wa kushoto wa Ufaransa Romain Perraud, 23. (Football Insider)

No comments