AIRTEL WAUZA MINARA YAO YOTE 1400 NCHI NZIMA
![]()
KUNA kitu hakiendi sawa sehemu? Wakati ikifahamika kuwa huduma ya simu za mikononi inaendelea kukua kwa kasi, kampuni ya simu ya Airtel inasemekana imeuza minara yake ya mawasiliano 1400 nchi nzima.
Minara hiyo imeuzwa kwa kampuni ya SBA kutoka Uingereza inayoongoza
duniani kwa kuendesha mifumo ya 'wireless' kwa dola za Kimarekani milioni 175
sawa madafu ya Tanzania bilioni 402.
Airtel, inayomilikiwa na kampuni ya Bhati Airtel iliyowahi
kutamba na Msudan Mo Ibrahim kama Celtel na kuwa 'The world's first borderless
network' Afrika Mashariki, imesema itatumia baadhi ya fedha hizo kulipia
madeni, kuongeza uwekezaji Tanzania na mgao kwa serikali ya Tanzania.
Dili hilo litamruhusu Airtel kuendelea na shughuli zake
kwenye minara hiyo lakini sasa akiwa amekodi nafasi.

Post a Comment